Friday, January 3, 2020

NEW LIFE IN CHRIST - ( MAISHA MAPYA NDANI YA KRISTO )

Posted by Savior Ministry at 2:06 AM 0 Comments


2 #Wakorintho 5:17-18
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.[18]Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
Nilipokuwa mchanga kwenye wokovu, niliambiwa haya ni matokeo ya Rohoni
( kuwa kiumbe kipya ) na hayako mwilini.
Inaweza kuwa ni kweli yenye Degree Fulani
( lakini kuna kweli kubwa zaidi ya Hii )
Kama huyu mtu amekuwa kiumbe kipya
Upya wake hautaonekana rohoni kwa macho ya nyama, kwasababu Watu hawawezi kuiona roho ila wanauona mwili , sasa yatakuwaje maisha mapya, atakuwaje kiumbe kipya kama mabadiliko hatutayaona mwilini ? Na Biblia inasema #Mathayo 5:16
[16]Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Upya huu una mabadiliko ya Jumla
Siku ileile mtu anapookoka ( Roho inapopokea upya, inapeleka taarifa ya mabadiliko sekunde ileile mwilini ). Ndio maana mtu akiokoka siku hiyo , ukimwambia ukazini atakataa, kwasababu hata mwili wake unaitikia mabadiliko.
Luka 19:8-9
[8]Zakayo akasimama, akamwambia Bwana, Tazama, Bwana, nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimenyang’anya mtu kitu kwa hila namrudishia mara nne.
[9]Yesu akamwambia, Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu.
Haya ni mabadiliko ya Zakayo baada ya kumpokea Yesu, ni siku hiyo hiyo , siku hiyo hiyo akawa mtoaji, siku hiyo hiyo kajua faida za kuwapa maskini, siku hiyo hiyo akaona sio vyema kukaa na vitu vya utapeli na unyang'anyi
Yesu akadhibitisha kuwa #Kweli wokovu
Umeingia #Ndani yake na nyumbani kwake.
( Haya yalikuwa ni mabadiliko ya Jumla)
Kwa mfano huu wa Zakayo utajua kuwa
Siku Mtu ameokoka kunakuwa na mabadiliko
Ya moja kwa moja kwenye Roho, Nafsi na Mwili.
KUNA KITU HUWA NAKIKATAA
mfano mtu ameanguka dhambini halafu
Watu wanasema ni mchanga kwenye wokovu,
Huu ufahamu sio mzuri sana endapo ukipewa kipaumbele.
Kwa mtu aliyeiamini kweli kwa kupokea injili ya kweli yenye uvuvio wa nguvu za Roho wa Mungu na akapokea mabadiliko kutokea kwenye maamuzi yake yaliyozaliwa na imani yake kwa Bwana Yesu ( Hawezi kufanya dhambi tena). Huyu ni kiumbe kipya.
ANGALIA HUU MSTARI KWA UMAKINI
2 #Wakorintho 5:17-18
[17]Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita #tazama! Yamekuwa mapya.
Ya kale yamepita #Tazama ! Yamekuwa Mapya
( angalia nyakati - Biblia inasema yamekuwa)
Uzito wa mstari huu ni haya maneno
#TAZAMA
#YAMEKUWA
Huyu mtu amekuwa kiumbe kipya
Mambo ya kale yamepita
Mambo gani ya kale
" Uongo , husuda, kutokusamehe, ugomvi, tamaa, wivu, ulevi , usengenyaji, uzinzi n.k "
Haya mambo biblia inasema yamepita ( sio yatapita baada ya kukaa kwenye wokovu miaka 3) , sio yatapita akianza kuhudhuria kanisani, No Biblia imesema yamepita. Haya mambo sio sehemu ya maisha mapya hata asilimia 0.000001
Biblia inasema #TAZAMA
( Hili Neno ndio limebeba maana ya Mstari kwa ujumla), Maana usipotazama " hutaona matokeo yeyote japo tayari yamekuwa mapya tayari.
TAZAMA ! YAMEKUWA MAPYA
Kuna maana kwanini Mtume Paulo alisema #TAZAMA, kiingereza imetumia Neno Behold " likiwa na maana kukiangalia kitu kwa muda na kwa umakini mpaka upate fundisho au ufahamu juu hicho kitu.
Hicho ndicho kinachosemwa kwenye kitabu cha mithali ; Mithali 24:32
[32]Ndipo nilipoangalia na kufikiri sana;
Naliona, nikapata mafundisho.
Ukitazama Na Kufikiria ukajua Yesu alisema IMEKWISHA
Yohana 19:30
[30]Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema,#Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
IMEKWISHA " maana yake nimekwisha kushughulikia chanzo cha anguko la mwanadamu, kwahiyo sasa mnaweza kuishi maisha huru"
Kama Bwana Yesu alikwisha kuishughulikia dhambi basi inawezekana kuishi mbali na husuda , chuki, visasi, uzinzi, tamaa
Ndio maana Biblia inataka UTAZAME
ufikirie kwa undani kile ambacho tayari Bwana
Yesu alikwisha kufanya kwa ajili yako UTAJUA KUWA yote yamekuwa mpya.
KUBWA KULIKO
Baada ya kutazama na kuona kuwa yamekuwa mapya Biblia inasema [18]Lakini vyote pia #vyatokana na Mungu,
VYOTE VYATOKANA NA MUNGU
baada yakuokoka na kuwa kiumbe kipya #SASA mambo yote yanatokana na Mungu
Afya yako haitokei kwenye dawa, Afya yako inatokana na Mungu , Ndoa yako inatokana na Mungu, Uchumi wako unatokana na Mungu , masomo yako yanatokana na Mungu, Huduma yako inatokana na Mungu ( HAKUNA TENA UGUMU WA MAISHA - KWASABABU VYOTE VYATOKANA NA MUNGU)
Unaacha kujitumainia mwenyewe unaanza kumtumaini Mungu aliyeweka Upya kwenye kila eneo.
Kuwa na Afya inakuwa jambo rahisi, kufanikiwa inakuwa jambo rahisi , Kuoa au kuolewa inakuwa jambo rahisi, Kuishi maisha maisha matakatifu inakuwa rahisi, kusamehe inakuwa rahisi kwasababu vyote vyatokana na Mungu.
UKIJUA HAYA UTAKUWA NA FURAHA YA
DAIMA YA WOKOVU
GOD BLESS YOU
Pastor Ibrahim Amasi
ABC - KAHAMA
LivingWord - 2019
" Make a Living "

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top