Bwana Yesu asifiwe!
Mara
nyingi katika maisha yetu huwa tunafeli na kukosea
shuleni,kazini,kwenye biashara,katika ndoa.n.k Hii ni kwa sababu
tunategemea akili zetu na maarifa yetu wenyewe.
Ebu tusome maandiko
Yohana 15:5
5
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake,
huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.
Hapa
tunapata majibu kwanini hatufanikiwi sababu Neno la Mungu ni amini na
kweli nalo lasema kwamba pasipo yeye(Yesu) sisi hatuwezi kufanya neno
lolote...hii ina maana wakati wowote tunapomuweka nje ya mipango na
maamuzi yetu...tumeamua kufeli au kushidwa.
Yamkini
ulitenda na kufanya mengi mwaka jana na hayakufanikiwa sababu ulimuacha
Yesu nje ila mwaka huu mualike ufanye naye na utaona mafanikio tele.
Utaona ukisoma Yohana 21:1-11
Utaona wanafunzi walivua samaki wakiwa peke yao na kukosa samaki lakini alivyokuja Yesu walipata samaki...
Kwanini?
Kwa sababu Yesu alivyokuja aliwapa Direction(MWELEKEO) aliwaambia katika mstari wa 6 tupeni jarife katika upande wa kuume....
Sijui unaona kitu hapo!!!
Yeye Yesu akiwa na wewe atakupa mwelekeo wapi upite wapi usipite nani uhusiane nae nani usihudiane nae...
Tunamuhitaji huyu Yesu maana bila mwelekeo hatutaweza fikia tunapotaka kufika.
Biblia inasema pasipo maono watu huacha kujizuia.
Yesu
anaijua kesho Yetu ebu mkabidhi njia zako aziongoze...mwambie atwae
miguu yako kwa uongozi wake...pasipo yeye mwenye maono tutashidwa
kujizuia na kufanya yasiyo tupasa na hivyo kushidwa kufikia hatma
zetu...
Mkabidhi Bwana njia zako pia umtumaini naye atafanya.
Mungu akubariki.
0 Comments: