Wednesday, January 20, 2016

NIA YA YESU KUJA DUNIANI ILIKUWA KUTUPA NAFASI YA KUTAWALA.

Posted by Savior Ministry at 12:38 PM 0 Comments
Bwana Yesu asifiwe, ninamshukuru Mungu kwa muda huu, na nafasi hii adimu ya kuzungumza na wewe kwa njia ya maandishi juu ya NIA YA DHATI YA YESU DUNIANI, hii inakuhusu wewe uliyeokoka, ambaye hujaokoka na ambaye uliokoka lakini ukarudi nyuma. 

Ukweli ni kwamba Mungu anafanya kazi na wote wampendao, nao ndio watendao sheria zake na kuzifuata, hao ndio waongozwao na Roho wake, uwepo wake unakuwa juu yao. 

Lakini dhambi baada ya kuingia duniani ilituondolea nafasi tuliyokuwa tumepewa baada ya Adamu kula tunda alilokatazwa, hivyo ikambidi Yesu aturejeshee ile nafasi kupitia Damu yake inenayo mema. 

Leongo la ujumbww huu ni kukutazamisha hii mistari michache ili uone nia ya dhati ya Yesu ya kuturejeshea nafasi, embu sema NAFASI, NAFASI. 

Neno la Mungu katika biblia linatupa uhakika ya kuwa tunapokuwa katika Kristo Yesu tunapewa nafasi ya kuwa
1. WAFALME
2. MAKUHANI

Hizi kimsingi ni nafasi mbili tofauti zinazofanya kazi tofauti tofauti. 

Ufunuo 5:9-10
''Ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na jamaa na taifa, ukawfanya kuwa UFALME na MAKUHANI kwa Mungu wetu, nao wanamiliki juu ya nchi''

Kwa maandiko haya yananipa picha kubwa ya uhalisia ya kuwa mambo kadhaa
Jambo la kwanza. 

Nafasi ilipatikana kwa njia Damu ya Yesu iliyotumika kama njia ya Transaction ili upate NAFASI, biashara ilotumika upate hiyo nafasi ni DAMU ya Yesu. 

Jambo la pili. 

Kila anayeitwa Mtu kutoka kabila lolote YESU hakwepeki, 

Kwa nini hakwepeki? Ile Damu haikubagua Kabila, Dini, Dhehebu, wala Rangi, wote tulinunuliwa kwa hiyo Damu, 

Ukimkubali tu unapewa nafasi ya UFALME na ukuhani kwa ajili ya kumiliki na kitawala kwa njia ya Yesu Kristo. 

Ufunuo 1:5-6
''..... Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake, na kutufanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu. 



kimsingi katika hali ya kawaida kufanyika mfalme na kuhani kwa wakati mmoja ni jambo kubwa na la heshima sana ambayo Mungu anampa mtu katika ya watu wengine ambao hawajaokoka ili huyo mtu atawale na kumiliki na Kristo. 

Sisi ni warithi pamoja na kristo Yesu. 

Sisi ni watawala pamoja na Kristo Yesu. 

Hatukustahili ili tulistahilishwa kwa agano la Damu ya Yesu ili tumiliki na kutawala na Kristo Yesu, 

Baada ya dhambi kuingia ulimwenguni ile nafasi tuliyokuwa tumepewa kupitia Adam wa kwanza aliipoteza ndiyo maana akafukuzwa kwenye bustani ya EDEN, hii ikaondoa uhalali wa kumiliki na kutawala. 

Usitegemee umetenda dhambi Halafu utukufu wa Bwana uwe juu yako, IKABODI.
Adam wa pili amerejesha sasa nafasi iliyokuwa imepotea. 

Kama hujaokoka wokovu upo kwa ajili yako, mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, usikubali kuingia mwaka 2016 ukiwa bado hujaokoka, wokovu ni sasa na si kesho, OKOKA LEO. 

Na Mwl David Sedekia
P. O. Box 1652
Dodoma
Tanzania.

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top