Sunday, September 6, 2015

UJUE UMUHIMU WA MLAWI KWAKO.

Posted by Savior Ministry at 8:09 AM 0 Comments
 Lawi ni kabila moja wapo katika mabila 12 ya Israel, Mungu alilichagua hili kabila na hawa watu ili watumike pamoja na Kuhani Haruni mara tu baada ya watoto wawili wa Haruni kufa, kabila la Lawi halikujichagua bali Mungu ndiye aliyelichagua ili kutumika, Mlawi yupo kuachilia utumishi ndani yako, Mlawi ni Mlezi kwako, Mlawi ni Baba wa Kiroho, Mlawi yupo ili afanye Mapenzi ya Bwana, yeye ni Fungu la Bwana, shauku yake nikuona utumishi wa watu walioitiwa ukisogea mbele, Lawi ni Lawi hawezi kuwa Reubeni isipokuwa anabaki kuwa Lawi. Sasa Mwl ninawezaje kumfahamu Mlawi wangu? Fuatana na mimi hapa chini; 
1. Ana nafasi kubwa sana ndani ya moyo wako 

2. Unampenda sana kumpokea ndani ya moyo wako.

3. Anakuwa sehemu ya Familia yako, kumbu kumbu la Torati 16:11. 

4. Anaachilia Roho ya Utumishi ndani yako. 

5. Anaachilia shauku yakumtumikia Mungu katika kizazi chako na kila neno analolisema ndani ya maisha yako linakuwa halisi na kutokea kwako.

6. Umefanikiwa kwa ajili ya maombi yake. 

Samwel alikuwa Mlawi kwa Sauli Mfalme wa Israel, Daudi na hata kwa wana wa Israel wote,

kwanini Mlawi?
Ameunganishwa na Utumishi wako, Ukiwa karibu naye unasogea kiroho, ukiwa mbali naye unakwama Kiutumishi. 
wewe unafikiri kwanini Mfalme Saul aende mpaka Makabulini kumtafuta Mlawi wake huku akiwa anajua tayari kashakufa? 

1Samwel 28:15, Hakika alikuwa kashachelewa kabisa, JILINDE USIMSAHAU MLAWI WAKO

 Katika kitabu cha Kumbu kumbu la Torati 16:19 maandiko yanasema, 
''Jilinde nafsi yako, usimwache Mlawi siku zote uishizo katika nchi yako'' 

Jihadhari maana yake, Jilinde, kuwa mwangalifu kwa namna yeyote, kuwa makini sana usimwache. 

Usimsahau katika kuinuliwa kwako popote usimuache kabisa, usimsahau maana nifungu la Bwana kwako, ukimpokea umekaribisha Roho ya Utumishi ndani yako. 

Hesabu 3:11-12, Kisha Bwana akanena na Musa na kumwambia, Mimi, Tazama nimewatwaa walawi na kuwatoa kati ya wana wa Israel badala ya wazaliwa wa Kwanza wote wafunguao tumbo katika wana wa Israel, na hao walawi watakuwa wangu. 

Mungu kawatwaa maana yake kawachukua, kuwatoa maana yake amewatenga kwa kazi maalumu tofaut na wengine, 

Hesabu 3:5-7, wamewekwa ili watumike pamoja na Haruni, pia watumike Maskani ktk utumish wao, Maskani maana yake ni uweponi mwa BWANA, 

Ufunuo 21:3, ''.....Tazama maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu..'', 

wao Kazi yao na shauku yao ni kuachilia Roho ya Utumishi ndani ya watu wa Mungu, 

ZOEZI (QUIZ) JIBU KWA Dakika 5 na ukusanye ndani ya moyo wako ili Roho Mtakatifu akusahihishie. 

1. Je wewe ni Mlawi? 
2. Je unamfahamu Mlawi wako? 
3. Je Upo karibu kwa kiasi gani na Mlawi wako? 
4. Je unamkumbuka Mlawi wako? 
5. Je unamuombea Mlawi wako? 
6. Je unamkumbuka Mlawi wako kama mwanzo? Au ulipofanikiwa uliendelea kumkumbuka au ulimsahau? Kumbu 12:19 Jilinde nafsi yako usimwache Mlawi siku zote uishizo ktk nchi yako. 

Ukisha sahihishiwa ukajikuta umekosea sana Toba ndiyo mlango kwako na umtafute leo Mlawi wako katika jina la Yesu ili utumishi wako uzidi kusonga mbele. 

Na
Mwl David Sedekia 
S. L. P 1652
 Dodoma Tanzania.

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top