Wednesday, January 15, 2014

KWA WATUMISHI WANANDOA NA WENYE UTUMISHI WANAOJIANDAA KWENDA HUKO!

Posted by Savior Ministry at 3:51 AM 0 Comments


YESU, MKE/MME, WATOTO HALAFU HUDUMA [WITO NA UTUMISHI WAKO]

-YESU
Unamhitaji Yeye Kwanza Kwa Ajili Ya U-MILELE WAKO (MAISHA YASIYOKUWA NA MWISHO BAADA YA KIFO); Lakini Unamhitaji Kwa Ajili Ya HEKIMA, UFAHAMU NA MAARIFA YAKE Yatakayokusaidia UWE BORA KWA MME/ MKEO, WATOTO (FAMILIA) NA HUDUMA [WITO NA UTUMISHI WAKO] Katika Maisha Yako Ya Hapa Duniani!

-MME/ MKEO
Kabla Haujasema Kwa Yeyote Kwamba Wewe Ni MKRISTO (MWANAFUNZI WA YESU) Na Mtumishi Wa Mungu; SHAHIDI WAKO WA KWANZA NI MME/ MKEO... HUDUMA YAKO YA KWANZA NI USTAWI NA UIMARA WA NDOA YAKO... NDOA YAKO IKIKWAMA; MWENENDO NA TABIA YAKO KAMA MWANAFUNZI WA YESU UKO MASHAKANI!

-WATOTO WAKO [FAMILIA]
Utawezaje Kumwambia Jirani Yako Atoe BORITI Jichoni Mwake Ilhali Unacho KIBANZI Jichoni Mwako??
Namna UNAVYOWALEA NA KUWAKUZA WANAO "KATIKA NJIA IWAPASAYO" Ndivyo UNAVYOPATA UBORA NA VIGEZO VYA KULEA WENGINE KWENYE HUDUMA [WITO NA UTUMISHI ULIOITIWA]!

-HUDUMA [WITO NA UTUMISHI ULIOITIWA]
Kinakuja Mara Baada Ya Kuwa Umefanya Vizuri Kwanza Kwenye MATATU YA KWANZA, Ukikwama Huko Na Hiki Nacho Kitakwama Au Kufa Kabisa!
KAMA UHUSIANO WAKO NA YESU NI MBOVU; HEKIMA, UFAHAMU NA MAARIFA YA KIMUNGU YATAKUPIGA CHENGA NA UTAKWAMA KIHUDUMA!
Kama Mahusiano Yako Mme/ Mke Hayako Sawa, HUDUMA ITAKWAMA AU KWENDA KWA SHIDA; ADUI UNAYEISHI NAYE NI MBAYA ZAIDI!
Mahusiano Yako Na Watoto Wako (Familia Yako) NA TABIA YAO NA MWENENDO WAO MBELE ZA WATU, UTAIFANYA HUDUMA YAKO ISIMAME AMA IANGUKE AU KUSUASUA!

Mwl D.C.K
dicoka@rocketmail.com
+255 655 466 675
+255 753 466 675


Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top