Sunday, January 27, 2013

MIUJIZA ITOKANAYO NA MAOMBI YA IMANI BADO IPO, SOMA USHUHUDA HUU!

Posted by Savior Ministry at 1:42 AM 0 Comments

Mwaka Jana Mwezi Wa Pili, Dada Mmoja Aliyesoma Hadi Ngazi Ya Masters Kwenye Maswala Ya Human Resource Alinijia Akiwa Na Hitaji Moja Tu; Ametafuta Kazi Kwa Karibu Miaka 2 Na Nusu Pasipo Mafanikio. Na Alishapeleka Sehemu Nyingi CV Yake Na Maombi Ya Kazi Lakini Hakuwa Na Jibu Lolote La Kuridhisha!
Baada Ya Kuniambia Hali Yake, Nilimuuliza Swali Rahisi, "Unaamini Yesu Anaweza Kufanya Nini Katika Hili?" Akanijibu Akasema, "Najua Anaweza Kunipa Kazi, Anaweza Kunisaidia Katika Hili"
Baada Ya Hapo, Nikakaa Naye Kwa Kama Nusu Saa Hivi, Nikamfundisha Mambo Mawili Matatu Kuhusu Haki Zake Katika Kristo Kama Mwana Wa Mungu, Na Kile Ambacho Maombi Ya Mwenye Haki Yanaweza Kufanya! Tulipomaliza Yale Maongezi, Nikamwomba BWANA, Na Nikamwamuru Adui Atoe Mikono Yake Juu Ya Maisha Ya Yule Dada Na Hatma Yake, Halafu Nikamshukuru Mungu Kwa Muujiza!
Nikamwambia Yule Dada, "Wakati Ninaomba, Nimezisikia Nguvu Za Mungu Zinapita Kwa Wingi Na Kwa Nguvu Ndani Yangu, Imekuwa Na Umepata Haja Ya Moyo Wako"
Wiki Mbili Baada Ya Maombi Yale, Yule Dada Alinipigia Simu Na Kuniambia, "Mtumishi, Nimepigiwa Simu Kutoka Wizara Ya Viwanda, Wamesema Niende Jumatatu Kusaini Mkataba Na Kuanza Kazi, Hakuna Hata Cha Interview"
Nikamuuliza, Ulipeleka CV Yako Huko Wizarani Lini? Akanijibu, "Mtumishi Yaani Sielewi, Nimepeleka Hiyo CV Tangu Mwaka 2010 Mwezi Wa Pili, Ni Miaka 2 Kamili Imepita, Namshangaa Tu Mungu"
Hivi Kweli, Inawezekana Kwa Wizara Kutojaza Nafasi Ya Kazi Kwa Miaka 2? Ilikuwakuwaje Wakakaa Miaka 2 Bila Kumpa Kazi Huyu Dada? Na Je, Wizara Gani Inaweza Kutoa Kazi Kwa Mgeni, Tena Bila Kumfanyia Hata Usaili? Hapa Ndipo Tunaporudi Kwenye Ukweli Usiopingika; MKONO WA MUNGU Ndio Uliyafanya Hayo!
Haijalishi Umesumbuka Au Kuhangaika Au Kuteseka Kwa Muda Gani Kwenye Changamoto Uliyonayo... Kama Umemwomba Mungu, Tena Kwa Imani Pasipo Mashaka, Kesi Yako Imeisha... Imekuwa, Imefanyika, Ni Swala La Muda... "IJAPOKAWIA INGOJE, MAANA NI KWA MUDA ULIOKUSUDIWA, HAKIKA HAITASEMA UONGO...ITAKUWA TU"
Na Iwe Kwako Kama Ilivyokuwa Kwa Huyu Dada Katika Jina La Yesu Aliye Hai... Mungu Akufute Machozi, Mungu Akukumbuke!
Tags:

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top