Sunday, January 27, 2013

DALILI ZA KUONESHA KUWA MKRISTO FULANI ANAKUA KIROHO AU HAPANA!

Posted by Savior Ministry at 1:30 AM 0 Comments
Na Mwalimu Dickson Cornel Kabigumila


1.Upendo Wake Kwa Mungu Unapanda Kila Iitwapo Leo (Mathayo 22:37-39):
Anazidi Kumpenda Mungu Kwa:
A.NGUVU ZAKE; Yuko Tayari Kujituma Kufanya Kitu Cha Kimungu Kinachohitaji Nguvu Yake... Atajituma Kufanya Usafi Kanisani, Mfano Kusafisha Viti, Kudeki Kanisa, Vyoo Vya Kanisa, Kusafisha Viwanja Vya Kanisa, Kusaidia Usafi Nyumbani Kwa Mchungaji,Kumfulia Mchungaji Nguo Au Kumnyooshea Nguo Zake... Kila Mmoja Anaweza Kufanya Haya Kama Akiamua Kufanya Kama Kwa Bwana... Muda Wote Yuko Tayari Kuitumia Nguvu Yake Kwa Ajili Ya Shughuli Za Kuujenga Ufalme Wa Mungu!

B.MOYO WAKE: Inapofikia Hatua Ambako Maslahi Ya Ufalme Wa Mungu Yanaujaza Moyo Wa Mtu, Hata Kufikia Hatua Kuvuka Mipaka Ya Udhehebu, Maadamu Kinahofanyika Ni Cha Ufalme Wa Mungu... Mtu Huyu Anakuwa Amekua Katika Kumpenda Mungu Kwa Moyo Wake. Raha Yake Inakuwa Katika Kuyafanya Yale Yaliyo Ya BWANA... Hiyo Ndo Furaha Ya Moyo Wake.

C.ROHO YAKE: Inapofikia Mtu Amekua Katika Ushirika, Ukaribu Na Mungu... Muda Wake Mwingi Anaoupata Atautumia Kwa Ajili Ya KUOMBA Na KUSOMA NENO Au Kujiudhurisha Mahali Pa Mafundisho Au Ibada... Mtu Ambaye Haya Yamepungua Au Yamekatika; Ameporomoka Kiroho, Amerudi Nyuma Na Muda Wowote Isipofanyika Juhudi Atakufa KIROHO

D.MALI YAKE: Biblia Inatuhamasisha Juu Ya ULAZIMA NA UMUHIMU WA Sadaka Na Matoleo Ya Aina Mbalimbali. Mtu Aliyefuzu Kiasi Kwamba Amejua Kuwa Mali Yake Ni Mali Ya Mungu... Yaani Yeye Na Mungu Ni WABIA Kwenye Kila Alichonacho, Kiasi Kwamba HAWEZI Kumzuilia Mungu Kile Anachomwagiza Moyoni Mwake ATOE... Huyu Mtu Tayari Amekwenda Hatua Kiroho, Amekua!

2.Ni Mwepesi Wa Kusikia, Ila Si Mwepesi Wa Kuongea
Huyu Mtu Amejua Kuwa KINYWA Chake Kimebeba Nguvu Ya UZIMA NA MAUTI... Hasemi Wala Kuzungumza Kila Neno Linalokuja Kwenye Mawazo Na Akili Yake... Anayachuja Maneno Yake Kabla Ya Kunena.

3.Hafanyi Maamuzi Au Hukumu Kwa Kuangalia Nini Anaona Au Anasikia (Isaya 11:3)
Mara Nyingi Atamuuliza Mungu Kuhusu Jambo Kabla Ya Kulitolea Maamuzi Au Hukumu, Ili Asifanye Kama Wanadamu Wa Kawaida

Nitaendelea Na Sifa Hizi Kwa Wakati Mwingine Kadri Mungu Atupavyo Muda Na Nafasi, Ubarikiwe Na Ufanikiwe!
Tags:

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top