Sunday, May 13, 2012

KANUNI NNE ZA KIROHO.

Posted by Savior Ministry at 8:15 AM 0 Comments

KANUNI NNE ZA KIROHO.
Kila jambo maishani lina kanuni zake. Kadhalika maisha ya kiroho yana kanuni zake za jinsi ya kushikiriana na Mungu.
KANUNI
·         MWENYEZI MUNGU ANAKUPENDA, NAYE ANAKAA KUKUPANGIA MPANGO WA AJABU KWA MAISHA YAKO.
UPENDO WA MUNGU
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yohana 3:16
MPANGO WA MUNGU KWAKO
Mimio nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10
·         MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI
Dhambi zake zimemtenga na Mungu. Kwa hiyo hajui upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yake.
MWANADAMU NI MWENYE DHAMBI
Kwasababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Warumi 3:23
·         YESU KRISTO NI NJIA YA PEKEE YA KUONDOA DHAMBI.
Alikufa kwaajili yetu ili tujue upendo na mpango wa kwa maisha yetu.
ALIKUFA ILI ATULETE KEA MUNGU
Kwa maana kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu.1 Petro 3:18
YESU YUHAI
Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa  atafufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko. 1 Wakorintho 15:3,4
YESU NDIYE NJIA YA PEKEE
Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi Yohana 14:6
·         INAKUPASA KUMPOKEA YESU AWE MWOKOZI NA MTAWALA WAKO. Ndipo utajua upendo na mpango wa Mungu kwa maisha yako.
UNAMPOKEA KRISTO KWA IMANI
Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake. Yoahna 1:12
Kwa maana mliokolewa ka neema, kwa njia ya imani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Waefeso 2:8,9
INAKUPASA KUMKARIBISHA YESU, MAISHA MWAKO
Tazama nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti uangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake...  Ufunuo 3:20
Kumpokea Yesu Kristo ni
·         Kujua wewe ni mwenye dhambi na kugeuka nafsi yakok kwa Mungu na kutubu
·         Kumtegemea Mungu kwa kukusamehe kabisa
·         Kumkaribisha Yesu Kristo atawale maisha yako kwa imani, ili uwe kama anavyokupenda
Je, ni picha gnai iliyo mfano wa maisha yako?
Je, ni picha gani ambayo ungependa iwe mfano wa maisha yako?
UNAWEZA KUMPOKEA KRISTO SASA
Mungu anaufahamu moyo wako, natena anakuwazia mema wakati wote sawasawa na Yeremia 29:19
Ifuatayo katika sala hii, inaweza kukusaidia kumpokea Kristo kuwa Mwokozi wa maisha yako, ukiomba kwa moyo wako wote

Bwana Yesu Kristo, ninakuhitaji, mimi ni mwenye dhambi. Nime kubali kwamba nimejitawala maisha yangu mwenyewe, na kutengana nawe. Asante kwa kifo chako msalabani kwaajili ya dhambi zangu na kwa kunisamehe zote. Sasa nageuka na kutubu. Bwana, nakuomba uingie ndani ya maisha yangu na kunitawala kabisa. Badili maisha yangu yawe upendavyo wewe, ingia ndani yangu uwe Bwana na Mwokozi wangu.
 
 
Tags:

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top