Friday, March 30, 2012

Vigezo vya kushiriki Gospel Star Search Vyatajwa!

Posted by Savior Ministry at 10:20 PM 0 Comments
Mwenyekiti na Mratibu wa Gospel Star Search Harris Kapiga

Gospel Star Search imerudi na tayari Vigezo vya kushiriki vimeshawekwa wazi. Akiongea na waandishi wa habari za Kikristo nchini, Harris Kapiga ambaye ni Mratibu wa shindano hilo alisema vigezi ni pamoja na 1. Awe Ameokoka 2.  Awe Hajatoa Albam Yake Sokoni 3. Umri Wowote Wa Mshiriki Utaruhusiwa. Na Vigezo Vingine vya ki-uweledi vitazingatiwa kwa ajili ya Kutunza nidhamu ya Washiriki Katika Mchakato huo.

Kapiga, aliendelea kusema “Tarehe 14 April, 2012 Kinyang’anyiro Cha Kuwasaka Washindi katika Kanda Ya Wilaya Ya Temeke Kitafanyika katika Ukumbi wa Saba Saba Opposite na Banda la Maonesho ya Biashara la Ofisi Ya Waziri Mkuu. Mchakato Utaanza Saa 3 Kamili.Tarehe 21 April, 2012 Jopo la Majaji Litaamia Katika Wilaya Ya Ilala Katika Ukumbi wa Msimbazi Centre Kuanzia Saa 3 Kamili asubuhi Washindi 30 Watakuwa wakitafutwa.

Washiriki Wengi Wilaya Ya Kinondoni Kinyang’anyiro Kitafanyika katika Hotel ya Etina Eneo la Survey Karibu na Mlimani City Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi.

Harris Kapiga ameendelea kutabanisha kwenye Blog ya Papaa kwa kusema kuwa Tarehe 2 Mwezi wa May, 2012 Kuanzia Saa 3 Kamili Asubuhi Katika Mikoa ya Mbeya, Iringa, Songea, Musoma, Mwanza, Kigoma, Tanga, Arusha na Kilimanjaro. Zoezi la Kuwasaka Nyota Wapya wa Muziki wa Injili litafanyika Kwa mpigo. Mara baada ya Washindi Kupatikana katika mikoa hiyo wataungana na Washindi wa Dar-es-Salaam na Kukaa Kambini kabla ya Kumsaka Mkali Mpya wa Muziki wa Injili Tanzania.

Kinyang’anyiro cha Gospel Star Search litafungwa rasmi 5 August, 2012 katika Jiji la Dar-es-Salaam, ambapo Mzizi Wa Fitina utakatwa siku hiyo.Kwa Watu Wanaotaka Kushiriki GSS 2012 na Mikoa yao hajatajwa basi wataombwa kushiriki katika Mikoa Jirani.

Tags:

Share This Post

Get Updates

Subscribe to our Mailing List. We'll never share your Email address.

0 Comments:

The Savior Ministry Live Chat

© 2016 Savior Ministry.
Powered by Themes24x7 .
back to top